Msanii Loan

MSANII LOAN

Huu ni mkopo unatolewa kufadhili Wasanii. Mkopo huu umekusudia kusaidia mahitaji ya vifaa vya kufanyia kazi kwa wasanii na pia hutumika kama mkopo wa kuleta suluhisho la kifedha kwa Msanii. Hivyo mkopo umegawanyika katika maeneo matatu ili kuweza kumsaidia msanii. Mikopo hiyo ni mikopo ya Pesa mikopo ya Pango na vifaa vya kufanya kazi (Vifaa

Mikopo ya Pesa
Lengo
Huu ni mkopo binafsi wa haraka wa kifedha wenye lengo la kuisaidia mahitaji ya muda mfupi kama vile malipo ya huduma mfano bili za maji na umeme, gharama za usafirishaji,na matibabu

Walengwa
Wasanii na mafundi wote wa sanaa za mikono kutoka viwango vya chini hadi vya juu kote nchini.

Kiasi cha Mkopo Kiwango cha mkopo ni kati ya Tsh.30, 000 mpaka 200,000 kitalipwa ndani ya muda wa miezi 6 na Kiwango cha mkopo ni kati ya Tsh.200,000  mpaka 5,000,000 kitalipwa ndani ya muda wa miezi 3 mpaka miezi 12

 

 

Mikopo ya Pango

Lengo

Huu ni mkopo binafsi wa kifedha wenye lengo la kusaidia mahitaji ya kodi, unaolenga kuboresha mazingira ya uzalishaji kwa wasanii kwa kuwakopesha kodi ili waweze kuwa na mazingira bora kufanyia kazi.

walengwa

Wasanii wote kutoka viwango vya chini hadi vya juu kwa nchi nzima.

Kiasi cha mkopo Kiwango cha mkopo ni kati ya shilingi 200,000  mpaka 3,000,000,kitalipa ndani ya muda wa miezi 12

Mkopo wa Vifaa vya kufanya kazi

Lengo

Huu ni mkopo wa kifedha wenye lengo la kusaidia mahitaji ya muda mrefu yenye kwa kuboresha mazingira ya uzalishaji kwa wa msanii kwa kukopeshwa vitendea kazi au vifaa.

Walengwa

Wasanii wote kutoka viwango vya chini hadi vya juu kote nchini

Kiasi cha Mkopo Kiwango cha mkopo ni kati ya shilingi 200,000 mpaka 500,000 kitalipwa ndani ya muda wa miezi 6 au miezi 3 mpaka 12

  • One
  • Two